Saturday, April 2, 2016

Dayna Aeleza jinsi anavyoweza Kufanya Muziki Bila Kuwa na Management

Ni wasanii wachache wa kike wenye uwezo ya kufanya muziki bila kuwa na management, lakini Dayna Nyange ni mmoja yao na ameeleza jinsi anavyoweza kufanya muziki mzuri bila kuwa na management.
Akizungumza na Djjonamusic Blog Jumatano hii, Dayna amesema kile kidogo anachokipata kupitia muziki wake, anakiweka ili kiendeshe muziki wake.

“Siko na management kabisa na hicho kitu nikikiongea watu wanashangaa, unawezaje?,” alisema Dayna. “Lakini siko na management kiukweli napambana mwenyewe tokea video yangu ya I DO, nilifanya mwenyewe na ilienda na ikaniongezea vitu vingi sana ndani ya Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Kwa hiyo ninachokifanya nikujibana katika kidogo nachopata nawekeza kwenye muziki wangu,” alisema Dayna.
Aliongeza, “Sema tu siwezi kusema kabisa niko mwenyewe kwa sababu kuna watu ambao nawategemea kwa namna moja au nyingine. Kwa hiyo ni heri kuwa na watu wengi wanao kusupport kuliko kuwa na manager mmoja ambaye sometime anakuangusha,”

No comments: