Siku kadhaa baada ya Shilole na
Nuh Mziwanda kuachana kulizuka tetesi na Nuh Mziwanda alikuwa
akilalamika kuwa msanii huyo alikuwa na mipango ya kutaka kumkwamisha
kimuziki kwa kumuwekea vizingiti mbalimbali, lakini baadaye Nuh Mziwanda
alisema kuachana na Shilole kumempa nafasi ya kujipanga vyema kwani
alidai kuwa ni kama alikuwa akitumika kimapenzi tu.
Malalamiko kutoka kwa Nuh Mziwanda hayakuishia hapo aliendelea kulalamika kwa mambo mbalimbali mpaka sasa alipotangaza ujio wa wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la 'Jike Shupa' Katika wimbo huo ambao amemshirikisha msanii Alikiba, Nuh anamzungumzia mwanamke ambaye hajatulia.
"Mimi siongei mengi kwa sasa wimbo 'Jike Shupa' ambao nimemshirikisha Alikiba, utaongea yaliyo moyoni mwangu"
No comments:
Post a Comment