Baada ya msanii Bright kuweka wazi
hisia zake kwa msanii Vanessa Mdee kuwa anampenda na anataka awe mke
wake kwa kumuoa kabisa, kauli hiyo imemtokea puani msanii huyo baada ya
binti aliyekuwa na mahusiano naye kumuacha.
Katika story 3 za Planet Bongo ya East Africa radio, amesikika binti huyo akiongea kwa simu na Bright ambaye alirekodiwa bila kujua, na kutoa kauli kuwa hamuhitaji tena aende kwa huyo huyo Vanessa Mdee.
Binti huyo ambaye hatukuweza kupata jina lake alisikika akisema kama hataki tena kuwa na mahusiano na msanii huyo ingawa bado anampenda, na kumtaka akamuoe Vanessa aliyemtaja kwenye media.
Bright ambaye ameachia wimbo wake wa 'Nitunzie' aliomshirikisha Baraka Da Prince, ambao pia ameu-dedicate kwa Vanessa Mdee, hapo jana alifanya interview na Planet Bongo, na kusema hadharani kuwa anampenda Vanessa Mdee, na yuko tayari kufanya chochote ili mradi amuoe awe mke wake rasmi.
No comments:
Post a Comment