Mchoraji maarufu wa vibonzo na mtangazaji wa Clouds FM, Masoud Kipanya amekiri kuwa misimu miwili iliyopita ya shindano la Maisha Plus ilipoteza mvuto kutokana na kuwachanganya vijana na akina mama na pia kuingiza masuala ya kilimo.
Na sasa Masoud amedai kuwa msimu mpya ambao tayari umeanza usaili utarudisha ile Maisha Plus ya awali yenye burudani zaidi.
“Msimu wa tano unarudi kwa vijana peke yao, hakuna tena kinamama, wakulima wala nani hawahusiki. Sasa hivi ni vijana peke yao. Kwahiyo ule mchakamchaka, ile burudani ya nguvu ambayo vijana walikuwa wanaipata kupitia Maisha Plus ya kwanza nay a pili sasa watakuja kuipata tena katika msimu huu wa tano,” Masoud alikiambia kipindi cha Super Mega cha Kings FM ya Njombe kinachoendeshwa na Divine Kweka.
Mwaka huu shindano litahusisha pia vijana kutoka Afrika Mashariki ambapo kutoka Tanzania watakuwa 14 na nchi zingine 16. Mshindi atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 30.
Msikilize zaidi hapo chini.
No comments:
Post a Comment