Mchekeshaji,rapper na Host wa Tv show ya “Wild ‘N Out” Nick Cannon anadaiwa kusita kutia saini nyaraka zinazoidhinisha talaka kati yake na aliekua mpenzi wake na mama wa watoto wake mwanamuziki Mariah Carey,aliedumu nae kwenye ndoa kwa miaka sita kabla ya wawili hao kutengana rasmi mwaka 2014 huku wakifanikiwa kupata watoto mapacha binti Monroe Cannon, na Moroccan Scott Cannon. ambapo haijabainika wazi sababu za uamuzi wake.
Mariah Carey(L) na Nick Cannon.
Gazeti laThe Sun limeripoti kuwa Nick Cannonmwenye umri wa miaka 35,amesita kutia saini nyaraka hizo zinazoidhinisha talaka kati yake na hit maker wa single ya “Touch my Body”huku tetesi zikidai kuwa badoNick Cannon anampenda Mariah Carey na amekua akiwaambia watu wake wa karibu kuwa Mwanamuziki huyo ni mwanamke sahihi kwake hivyo uamuzi wake una lengo la kukamwisha ndoa kati ya Mariah Careymwenye umri wa miaka 46 na bilionea raia wa Australia James Packer aliemvisha Mwanamuziki huyo pete ya uchumba on january 2015.
No comments:
Post a Comment