Monday, June 6, 2016

Shetta akanusha madai ya kusafirisha madawa ya kulevya.



Akizungumza na Enewz ya EATV, Shetta alikanusha tuhuma hizo na kudai kuwa shughuli kubwa inayomuingizia kipato ni muziki na kuongeza kuwa safari zake za nnje ya nchi muda wote zimekua kwa ajili ya ku-shoot videos na kufanya show.


Star huyo  Bongo Fleva  anayefanya vizuri na single yake mpya “Namjua” amebainisha wazi juu ya mafanikio yake baada ya tetesi kuenea mitandaoni kuwa ni miongoni mwa wasanii wanabeba mizigo ya “unga”(madawa ya kulevya) kutokana na safari zake za nnje ya nchi mara kwa mara hasa Afrika kusini.
“Mimi sifanyi hiyo biashara nafanya mziki kuna vitu vingi vya kutuingizia pesa sisi wasanii tunauza video zetu youtube,tunauza miito ya simu,kuna endorsement na nimeshakuwa balozi wa kampuni kubwa so nina vitu vingi vya kuniingizia pesa”,alisema Shetta.

No comments: