Thursday, September 8, 2016

Sony wapiga chini kwa muda usiojulikana tarehe ya kuachia video mpya ya Davido

Davido hajaachia wimbo wowote mwaka 2016 baada ya kusaini mkataba mnono na label ya Sony Music WorldWide, na inaonekana hatoachia wimbo wowote hivi karibuni.

image001-2
Sony ambao walisaini mkataba wa mamilion na staa huyo wa Nigeria, wamesogeza tena mbele tarehe ya kuachia wimbo mpya wa Davido aliomshirikisha Tinashe. Mkataba wao unaipa label hiyo haki ya kusimamia uachiwaji wa kazi zote za Davido, ikiwemo upangaji wa tarehe za kutoka kwa nyimbo zake.

Davido-Tinashe-1
Wimbo mpya wa Davido ‘How Long’ ambao tayari umekamilika kila kitu mwanzo ulipangwa kutoka Tarehe 9 mwezi huu,
I’m happy I waited, I’m about to turn up,Happiest day of my life, finally got my date of release. September about to be a movie, best music and videos I ever made in my life.”Davido aliandika kuonesha furaha yake baada ya kupangiwa tarehe ya kuachia kazi yake mpya kutoka kwa maboss wake wapya.
Davido-Snap-1
Lakini furaha hiyo imeingiwa na dowa siku moja kabla ya tarehe ya kuachia kazi hiyo, imeripotiwa kuwa Sony wameipiga tena kalenda tarehe ya kuachia kazi hiyo na Davido ameshindwa kujizuia, ametumia Snapchat kuonesha hisia zake



No comments: