Saturday, October 15, 2016

‘Formation Tour’ ya Beyonce imeingiza zaidi ya dola Million 256

Mapato yaliyopatikana kwenye ziara ya muziki ya Beyonce yametangazwa.Ziara hiyo ambayo ilianza April 27 huko Miami na kumalizika tarehe 7 Oktoba imeingiza zaidi ya dola Million 256,084,556 huku ikiwa imeuza tiketi zaidi ya Million 2.2.
Kwa mujibu wa Billboard kila show moja ilihudhuriwa kwa wastani wa watu zaidi ya 45,757 na kuingiza kiasi cha Dola Million 5.2.
Huku show ya London iliyofanyika kwenye uwanja wa Wembley ikivunja rekodi kwa kuingiza dola Million 15.2 na kuhudhuriwa na watu zaidi ya 142,5000.

No comments: