Monday, August 6, 2018

Roma Mkatoliki sio mchizi wangu kabisa, na wimbo wa Parapanda sijausikia – Moni Centrozone (+video)

Rapa kutoka Dodoma, Moni Centrozone amedai kuwa hana urafiki wowote na Roma Mkatoliki kwa sasa ingawaje walikuwa pamoja kipindi cha nyuma wakati wa tukio la kutekwa na watu wasiojulikana.Moni akiongea na Djjonamusic Blog amesema kuwa ameona hakuna msaada wowote kutoka kwa Rapa mwenzie Roma Mkatoliki na ndio maana yupo bize kupromoti wimbo wake mpya wa Utaprove.
 Akizungumzia kuhusu ngoma mpya ya Roma na Stamina (ROSTAM) inayoitwa Parapanda amesema kuwa wimbo huo haufahamu na hana haja ya kuufuatilia licha ya kufanya vizuri kwa sasa na badala yake yupo bize kupromoti wimbo wake mpya. Tazama full video hapa chini

No comments: