Shilole akiongea mapema leo kwenye tukio la wasanii kutembelea mradi wa SGR, amesema kuwa wasanii wawe kitu kimoja kwa kumsapoti Rais Magufuli kwa vitu anavyovifanya.
“Unajua unavyojichanganya na wenzio ndio unavyopata connections. Mtu ambaye anaitwa na kiongozi wako halafu hautii, hiyo sio heshima, it means huwezi kuheshimu wazazi wako. Unajua unavyoitwa na Rais huwezi jua anakuitia nini?je, akikuteua kuwa mkuu wa mkoa, au mkuu wa Wilaya utakataa?,”amefunguka Shilole na kumuomba jambo Rais Magufuli.
“Kwanza nataka nimuombe ombi Mhe. Rais Magufuli, nataka aniruhusu niuze chakula kwenye Treni itakapoanza kazi, mimi sitaki hela nataka tu anipe nafasi hiyo basi“
Credit by Bongo5.com
No comments:
Post a Comment