Baada ya kupokea kichapo kibaya cha jumla ya mabao 5 – 0 dhidi ya
Mafarao wa Misri klabu ya Al Ahly mwishoni mwa wiki, hatimaye
wawakilishi wa Tanzania Simba SC wameanza kurejea nchini kwa mafungu.
Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Simba zinasema kuwa baadhi ya
wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wamewasili salama nchini hapo
jana Februari 4.
”Baadhi ya wachezaji, benchi la ufundi na
viongozi walioambatana na timu nchini Misri wamewasili salama nyumbani
Tanzania,” imeripoti klabu ya Simba.
”Mabingwa hao wa ligi kuu
soka Tanzania Bara wameongeza ”Wachezaji waliobaki nchini Misri leo
(jana) mchana wamefanya mazoezi katika moja ya viwanja vilivyopo kwenye
hoteli ya Africana mjini Alexandria. Leo usiku wataanza safari ya
kurejea nyumbani Tanzania,”
Kundi hilo la pili limetarajiwa
kiwasili leo Februari 5, Mnyama Simba mpaka sasa amepoteza mchezo wake
wa pili mfululizo baada ya wakwanza kufungwa 5 – 0 dhidi ya AS Vita Club
ya DR Congo ikiwa ni michuano ya klabu bingwa Afrika hatua ya makundi.
Meneja
wa klabu hiyo Patrick Rweyemamu amesema sababu kubwa ya timu hiyo
kurudi kwa mafungu kulitokana na mabadiliko ya muda wa mechi, kwa sababu
hapo awali mechi ilipangwa kuchezwa saa 1 jioni lakini baadaye
ikabadilishwa na kupelekwa saa 3 usiku.
“Tulitegemea baada ya
mechi kumalizika watu warudi usiku ule ule ili wafike Dar es Salaam siku
ya Jumapili na kama wote tulivyopata taarifa tulitegemea mechi ichezwe
saa 1 ikaja kubadilishwa ikachezwa saa 3, kwa maana hiyo ratiba ya muda
wa kuondoka ilibadilika”
“Kwa hiyo kuna baadhi ya watu wataondoka
Jumapili ambao toka awali tiketi zao zilikuwa hazina matatizo na kuna
baadhi ya wachezaji wengi wataondoka Jumatatu” alisema Rweyemamu.
Simba
inatarajia kucheza mchezo wa marudiano dhidid ya Al Ahaly February 12,
2019 kwenye dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mpaka
sasa Simba inaendelea kusalia na alama zake tatu na kushika nafasi ya
tatu kwenye msimamo wa kundi D huku wakiwa wamebakiwa na michezo mitatu
ukiwemo mmoja pekee wa ugenini dhidi ya JS Saoura. Credit by Bongo5.com
No comments:
Post a Comment