Diamond akiwa na mtoto wake Tiffah.
Hatua hiyo imekuja baada ya wiki moja iliyopita baraza hilo kutangaza sheria mpya zinazowakata wasanii kuomba vibali wanapotaka kwenda nje ya nchi kwaajili ya show zao.
Basata wamesema sio kweli kwamba wamemtaka Diamond kuchukua kibali cha kwenda kuhudhuria birthday ya mtoto wake kama inavyoadiwa katika mitandao ya kijamii.
“Tunapenda kuutarifu umma kuwa taarifa inayosambaa kwamba Msanii Diamond anatakiwa kuchukua kibali BASATA kwenda kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa mwanaye si ya kweli,” wameandika Basata kupitia mtandao wao.
Waliongeza “Vibali vya wasanii kwenda nje havihusiani na safari binafsi. Tunazidi kuwakumbusha wasanii kufuata taratibu zote wanapoenda kufanya maonesho nje ya nchi.,”
Wiki moja iliyopita muimbaji huyo alizuiwa na Basata kwenda kufanya show nje kwa kuwa hakuchukua kibali cha kwenda kufanya show nje ya nchi lakini baadae aliweza kufuata taratibu za kuchukua na kusafiri.
No comments:
Post a Comment