Habarai mbaya zaidi kwa mabingwa hao wa Premier League ni kuwa Juventus sasa itaongeza juhudi zake za kumng’oa kocha wa klabu hiyo Pep Guardiola.
Manchester City ilijikuta ikiingia kwenye mtikisiko huo siku ya Ijumaa pale Bodi ya UEFA inayohusika na udhibiti wa matumizi ya fedha ilipoifungia kwa muda wa miaka miwili kutokana na matokeo ya uchunguzi kubaini kanuni na sheria hiyo kukiukwa.
Klabu hiyo kutoka Premier League inatarajiwa kubisha hodi huko kwenye mahakama ya usuluhisi ikionyesha kutoridhishwa na maamuzi yaliyotolewa.
Kwa mujibu wa The Sun, Miamba hiyo ya Hispania, Real tayari ipo kwenye mipango ya kutoa dau la paundi milioni 180, hii ikiwa ni kabla hata ya taarifa hizo za kushitua za kufungiwa kwa City.
Sterling mwenye umri wa miaka 25, ana kandarasi ya miaka mitatu ya kuwa katika dimba la Etihad huku mazungumzo yakiendelea tangu mwezi Novemba kuhakikisha anaongezewa mapato yake ya wiki kutoka paundi 300,000 hadi kufikia 450,000.
No comments:
Post a Comment