Tuesday, February 18, 2020

Waislamu nchini China wazuiliwa kufuga ndevu kufunika uso na kutimia Internet, Sababu zaelezwa

Stakabadhi iliyoonyesha jinsi China inavyowazuilia maelfu ya waislamu katika taifa hilo kutumia mitandao ya kambi maalum  pamoja na kufuga ndevu na kufunika nyuso imebainika.

Kwa kuorodhesha taarifa binafsi ya zaidi ya watu 3,000 kutoka eneo la magharibi la Xinjiang, nchi hiyo inafuatilia maisha ya kila siku ya watu.
Rekodi hizo za kina- zinajumuisha kurasa 37, safu na mistari- inaangazia jinsi watu wanavyoomba, wanavyovalia nguo, wanawasiliana na nani na mienendo ya familia zao.
China inakanusha kuwa hatua hiyo ni ya ukandamizaji, na kusema kwamba ni njia makhsusi ya kukabiliana na ugaidi na itikadi kali za kidini.
Stakabadhi hiyo inayosemekana kuvujishwa katika hatua ya kuhatarisha maisha, inatoka kwa chanzo cha habari ndani ya Xinjiang ambayo pia ilivujisha stakabadhi zingine za siri zilizochapishwa mwaka jana.
Mmoja wa wataalamu wakuu duniani kuhusu sera ya China katika eneo la Xinjiang, Dr Adrian Zenz, na mwanazuoni wa ngazi ya juu katika wakfu wa ukumbusho wa waathiriwa wa sera za kikomunisti mjini Washington, anaamni ufichuzi wa hivi punde ni wa kweli.

“Stakabadhi hii muhimu inafichua ushahidi wa hali ya juu ambao nishawahi kukumbana nayo hadi wa leo kwamba Beijing inawanyanyasa na kuwaadhibu watu kwa kufuata utamaduni na imani ya kidini”.
Moja ya kambi inayotajwa katika stakabadhi hiyo ya ufichuzi, inasema “Kituo cha mafunzo nambari nne” kimetambuliwa na Dkt Zenz kama moja ya zile zilizotembelewa na BBC kama sehemu ya matembezi yaliyopangwa na mamlaka za China mwezi Mei mwaka jana.
China imedaiwa kukamata Waislamu milioni moja ili kuzuia ugaidi
Baadhi ya ushahidi uliofichuliwa na BBC unaonekana kuambatana na stakabadhi mpya iliyovujishwa, ambayo imefutwa kwa wino baadhi ya sehemu kabla ya kushapishwa ili kulinda majina ya wale waliojumuishwa katika stakabadhi hiyo.
Inajumuisha taarifa za kina za uchunguzi wa watu 311 wanaodaiwa kuwa washukiwa wakuu, kwa kuorodhesha walikotoka, tabia zao za kidini, mahusiano yao, mamia ya jamaa zao, jirani zao na marafiki.
Uamuzi uliofikiwa na kuandikwa katika safu ya mwisho utaamua ikiwa wale ambao tayari wanazuiliwa waendelee kuzuiliwa au wachiliwe, na ikiwa baadhi ya wale waliokuwa wameachiliwa wanastahili kukamtwa tena na kuzuiliwa.
Ni ushahidi ambao unaonekana kukinzana moja kwa moja na madai ya China kwamba kambi hizo ni vituo vya mafunzo au shule.
Katika mchakato unaochanganua na kuhakiki stakabadhi hizo, Dkt Zenz anasema kuwa inatoa maelezo ya kina ya kuelewa sababu halisi ya mfumo huo wa udhibiti.
Inatoa maelezo ya ndani ya hisia ya wale wanaofanya maamuzi, alisema, inaweka wazi “Falsafa ya kiitikadi na utawala unaolenga kukandamiza uhuru wa kidini” katika kambi hizo.
Safu 598 inajumuisha kesi ya mwanamke wa miaka 38- ambaye jina lake la kwanza ni Helchem, aliyepelekwa katika kambi ya kuzuilia watu sababu kuu ya kukamatwa kwake: Alikuwa akivalia vazi la kidini linalofunika uso wake kwa miaka kadhaa iliyopita.
Ni moja tu ya idadi ya visa vya kuzuiliwa bila sababu ya msingi, na kuadhibiwa bila kufanya makosa.
Wengine walikamatwa kwa sababu ya kutuma maombi kutaka pasipoti- ishara kwamba hata kusafiri nje ya nchi sasa inachukuliwa kama dalili ya itikadi kati ya kidini katika eneo la Xinjiang.
RAMANI
Katika safu ya 66, mwanamume wa miaka 34-ambaye jina lake la kwanza ni Memettohti alizuiliwa licha ya uamuzi uliofikiwa kuonesha kuwa “sio mtu hatari”.
Halafu kuna huyu mwanamume wa miaka 28 anayefahamika kama Nurmemet katika safu ya 239, ambaye amewekwa kizuizini kwa “kubonyeza link kwenye mtandao na bila kujua na kujipata katika tuvuti ya kigeni”.
Pia, kesi yake inamuelezea kuwa mienendo yake haina tatizo.
Watu 311 wanaochukuliwa kuwa washukiwa wakuu wanatokea jimbo la Karakax, karibu na mji wa Hotan kusini mwa Xinjiang, eneo ambalo zaidi ya 90% ya watu ni wa kabila la Uighur.
Idadi kubwa ya Wauighur ni waislamu, wanafanana kwa muonekano, lugha na utamaduni wao ni watu wa eneo la kati mwa bara Asia kuliko jamii kubwa ya China, ambao ni kabila la Han.
Katika karne za hivi karibuni mmiminiko wa mamilioni ya watu wa kabila Han katika eneo la Xinjiang umeibui mzozo wa kikabila na hali ya taharuki imekuwa ikiongezeka.
Hali hiyo inasadikiwa kuwafanya watu wa jamii ya Uighur kutengwa.
Chanzo BBC.

No comments: