Tuesday, November 18, 2014

Majambazi Yaliyopora Katika Benki Ya Stanbic Yakamatwa

Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam limewakamata watu sita waliohusika katika wizi wa zaidi ya shilingi million 500, kaatika benk ya Stanbic tawi la Mayfair mnamo octoba 23 mwaka huu.Majambazi Yaliyopora Katika Benki Ya Stanbic Yakamatwa
Watu hao raia wa Kenya na watanzania watatu, akiwemo Meneja msaidizi Selestine Nalogwa Mkumbo, mtunza funguo Anastazia Frank Ringo na mpelelezi wa Bank hiyo Tegemea Ayoub ambao wamebainika kuhusika katika wizi huo.


Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam Kamishna wa Polisi Kanda Maaalum ya Polisi Suleiman Kova alisema, wafanyakazi wa benk hiyo waliohusika wamekamatwa kulingana na upelelezi wa jeshi hilo na majambazi wengine walikamatwa katika eneo la Mbezi Beach wakiwa wanapanga kufanya tukio lingine la Uporaji.

Aidha kamishna Kova alisema katika upelelezi uliofanywa na jeshi la polisi  umebaini kuwa    zaidi ya shilingi milioni 300 zilikwisha tolewa katika benk hiyo siku chache kabla ya tukio.

Katika hatua nyingine jeshi hilo limewakamata majambazi sugu kumi pamoja na silaha mbalimbali ikiwa ni mwendelezo wa oparesheni ya kupambana na uhalifu wa kutumia silaha na pikipiki iliyoanza octoba 28 mwaka huu.

No comments: