Tuesday, November 18, 2014

‘PANADOL YA WANAUME’ MATATANI UGANDA

Baada ya msanii wa kike wa Uganda Desire Lusinda kukutwa na sakata la picha za utupu hadi kufikia waziri wa maadili wa Uganda kuingilia kati na kutaka afikishwe kwehye vyombo vya sharia,  msanii mwingine wa muziki wa kizazi kipya nchini humo Kansiime Jemimah maarufu kama -Panadol wa Basajja- amepelekwa rumande baada ya kukanusha mashtaka ya kusambaza picha za uchi kinyume na sheria za nchi.
Mwanamuziki Kansiime Jemimah maarufu kama -Panadol wa Basajja.
‘Panadol wa wanaume’ ambalo ni jina la kisanii la mwimbaji chipukizi wa Uganda-Kansiime Jemimah amepelekwa rumande baada ya kukanusha mashtaka hayo.


Msanii huyo wa kike alikamatwa pamoja na mtengezaji wa muziki wake mwezi uliopita kwa kile waziri wa maadili anasema ni kuhusiana na picha za uchi.

Panadol ametoa vibao kadhaa katika mahadhi ya kufoka lakini ule ambao umemletea shida unaitwa Ensolo Yange yaani mnyama wangu.

Katika video ya wimbo huo kuna sehemu ambapo yeye mwimbaji akiwa kama mhusika mkuu anaonekana akivaa chupi ya G-string huku makalio yake yakiwa nje.

Na pia kuonyesha mapaja yake na baadhi ya maneno ya muziki wake yakiwa

Kwa baadhi wanatafsiri maneno na picha hizo vingine na serikali kusem ani kinyume na sheria.

Mwaka jana sheria mpya dhidi ya picha chafu ilipitishwa ambapo ni marufuku kuuza au kupatikana na picha za uchi. Adhabu ya mtu anaepatikana na hatia ni faini ya shilingi za Uganda laki mbili sawa na dola nane au kifungo cha miaka mine au vyote viwili.

No comments: