Wednesday, November 19, 2014

(Season 2) Top 5 ya watangazaji wanaozitengenezea Media zao mkwanja mrefu

(Nafasi tano) za watangazaji wanaozitengenezea media zao mkwanja wa kutosha na kufanya redio kujulikana zaidi na kuwasogeza wasikilizaji wengi zaidi na kumshawishi mdau kuweza kutangaza na redio husika.

(Utaratibu) huu utakua ni kwa kila j5 ya kila wiki na hii idea ni ya kwanza kabisa katika ulimwengu wa blog hapa Tanzania sio mbaya kama ukiona inafaa na kuindeleza kwenye chanzo chako Team Djjonamusic blog na Radio imekaa chini na kuona bora kuanzisha hizi chati.

(Kigezo) ni kuangalia na kufuatilia idadi ya matangazo yanayochezwa katika kipindi au show husika na uzito wa hayo matangazo.
Nafasi ya Tano imeshikiliwa na Millard Ayo ambaye ni mtangazaji wa Clouds fm  iliyopo hapa Dar na show ambayo anaiendesha inaitwa Amplifaya ni kila siku za wiki namaanisha j3 mpaka ijumaa.

Nafasi ya Nne amekaa  Eddo Bahir mtangazaji tokea Iringa kupitia redio Ebony fm na show ambayo ana host ni One six , Hii show ni kila siku za wiki time ni saa kumi na mbili mpaka Tatu kamili za usiku

 
Nafasi ya Tatu imekamatwa na Dokta joe huyu jamaa ni mtangazaji wa kituo cha redio cha Ebony fm iliyopo mkoani Iringa, jamaa anaendesha show inaitwa The splash hii show huluka kuanzia jumatatu mpaka ijumaa time ni saa saba na robo mpaka kumi kamili.
 
Nafasi ya Pili imeshikiliwa na Renatus Bizzo kiluvia ambaye ni mtangazaji wa Redio free Africa iliyopo jijini mwanza show inaitwa Showtime New chapter ni kila siku za wiki.
 

Na kwa hii wiki ya pili tena nafasi ya kwanza imeshikiliwa na B12 aka The navigator wote mnafaham uyu jamaa yupo pale Clouds fm show inaitwa XXL time saa saba kamaili mpaka kikumi kamili.

No comments: