Barnaba: Sio kama sipendelei kwenda International , natamani kuwa kama kina Youssou n’dour, 2 Face, Sauti Sol, lakini
Barnaba ni miongoni mwa wanamuziki wa
Tanzania waliojaliwa vipaji vingi kikiwemo cha uandishi wa nyimbo,
ambacho kimewafaidisha hata wasanii wengine akiwemo Vanessa Mdee ambaye
ameanza kufanya vizuri kimataifa. Kwa uwezo alionao Barnaba, wengi
walitarajia kuwa hadi sasa angekuwa amefika mbali zaidi ya hapo alipo,
hasa katika kujitangaza kimataifa ikiwa ni pamoja na kufanya collabo na
wasanii wa nje. Barnaba amezungumza na Bongo 5 na kutoa sababu za
kwanini hadi sasa hajaanza kuonesha jitihada za kwenda kimataifa. “Watu
wengi wanaamini kwamba Barnaba ana package ambayo inajitosheleza kwenda
International, na mimi mwenyewe naamini kuwa nina package ya kutosha
ukizingatia watu wanavyoni include, Barnaba mwandishi, composer,
muimbaji, Barnaba ana studio yake. Ofcourse kweli ni maamuzi na
kuna
kujipanga, Sio kama siumii na sio kama sipendelei, ofcoz hata mimi
mwenyewe nahitaji kuwa International lakini International mwenye package
ya kujitosheleza.” alisema Barnaba. Ameongeza kuwa anatamani kuwa kama
wasanii wakubwa wa Afrika lakini kutokana na malengo yake ya kutaka
kuliteka kwanza vizuri soko la nyumbani ndio maana mpaka sasa bado
hajaweka nguvu nyingi kwenda kimataifa. “Mi natamani kuwa kama kina
Sauti Sol, natamani kuwa kama Kina Maurice Kirya, kina Youssou n’dour,
kina Lokua Kanza, kina P- Square, 2 Face, natamani kuwa lakini sio
kwamba siwezi naweza lakini nafikiri mkakati wangu unaenda taratibu
taratibu, package yangu ilikuwa kwanza kushawishi nyumbani wanielewe
kwenye package ambayo inajitosheleza, naamini nyumbani wamenielewa
lakini kuna kiasi ambacho sijatosheka nacho.” “Safari ya kwenda
International iko tayari na imeanza lakini hakuna kitu kizuri kama
kufanya ukaonesha watu kuliko kuzungumza kwa watu, niko kwenye kufanya
niwaoneshe watu nitakapokuwa tayari kuwaonesha wataona. Kwa sasa hivi
nafanya album yangu ambayo itavuka International ukizingatia video, kuna
wasanii ambao nimewashirikisha wengi ni International mule ndani"
alisema Barnaba.
No comments:
Post a Comment