Christian Bella, Ally Kiba kuachia ngoma baada ya Ramadhani
Ile collabo kali
iliyokuwa inangojewa kwa muda sasa kati ya Christian Bella na Ally Kiba
inatarajiwa kutoka baada ya mfungo wa Ramadhani. Akiongea na Sasa TV,
Christian Bella amesema kuwa wimbo huo utakuwa ni wa kipekee kwani Ally
Kiba amebadilika humo ndani na kuimba tofauti kitu kilicholeta radha
tofauti ya wimbo huo. Bella ameongeza kuwa Ali Kiba ameimba kwa kupanda
na kushuka kama yeye kitu kilichomfanya aipende kazi hiyo ambayo mpaka
sasa jina lake halijajulikana. Aidha Christian Bella amesema kuwa kwa
sasa wanajipanga kushoot video ya wimbo huo na mpka ramadhani iishe
video hiyoitakuwa tayari na ndio utakuwa wakati mwafaka wa kuachia ngoma
hiyo ambayo mpaka sasa audioyake ipo tayari.
No comments:
Post a Comment