Jacqueline Wolper Atoa Wosia Mzito, Ahofia Kifo >>>>>>>>
Msanii wa filamu nchini Tanzania,
Jacqueline Wolper , ameonyesha hofu ya Mungu baada ya kujikuta akiwaza
na kutafakari juu ya kifo jambo ambalo amedai kuwa limemyima usingizi na
kujikuta akilia na kuwataka watu walio na tofauti au waliopo kwenye
migogoro uweza kusameheana ili lolote likitokea waweze kuiona pepo.
Kupitia mtandao wa kijamii ameandika “Nimelala lakini hakulaliki nipo
tuu natafakari kitu kinaitwa kifo, watu wa dini wanasema usilie bali
uombe kwa Mungu apunguziwe adhabu ukilia
unamuumiza sijui unamzidishia
adhabu sasa mtu unaumia ufanyaje?”. “Jamani dah kifo bwana acheni tuu
Mungu aitwe Mungu lakini pia silaumu ila naamini Mungu kafanya hivi ili
pia tusijusahau natumkumbuke kuwa yeye yupo sasa ndugu zangu mliogombana
mlioachana kimapenzi embu mtafute mwenzio msemezane tuu ata kwa salamu
mkikutana ili akifa uweze kwenda kumtilia mauwa au kumuaga”. Akamalizia
“Niwazo tuu nimetoa nanimeona ni share na nyinyi followers wangu
nawapenda sana nawatakia usiku mwena mliopo kwenye starehe muendeshe
magari taratibu mrudipo majumbani mwenu namsilewe sana …Bad mood wallah
nalia pekee yangu Mungu nipe nguvu. ndugu zangu,marafk vipenzi,jamaa
wote mliotutangulia Mungu awapunguzie adhabu one love”
No comments:
Post a Comment