Faiza aikatia rufaa hukumu ya kupokonywa mtoto na Sugu >>>>>>>
Aliyewahi kuwa mchumba wa mbunge wa Mbeya
mjini Joseph Mbilinyi aka Sugu, Faiza Ally amesema ataikatia rufaa
hukumu ya kupokonywa mtoto waliyezaa pamoja iliyotolewa wiki hii. Faiza
amesema haamini kama kuna sheria inayosema mama atakanyakanywa mtoto
kutokana na nguo zake anazovaa. “Nasitikishwa sana na maneno yenu makali
hasa nyinyi mnaosambaza kashfa juu yangu kuhusu mavazi yangu,”
ameandika kwenye Instagram. “Hakuna hiyo sheria Tanzania inayosema
nipokonywe mtoto kuhusu mavazi yangu- nimekata rufaa na nawahakikishia
nitashinda kesi na nitamlea mwanangu na nitavaa mavazi yangu na nita
enjoy maisha yangu/ nina mwanasheria makini aliyesomea sheria na sisi
nyinyi mnao nipa hukumu humu ndani na kwingine,” ameongeza. “Pamoja na
mavazi yangu mimi ni mama bora! mnajua upande wangu lkn hamjui upande wa
Sugu na hakika mengi mtayajua kupitia kesi hii/ mavazi yangu nayapenda
na kwa mujibu wa sheria si kitu kinacho nifanye ni pokonye mtoto wangu-
maneno yenu machafu dhidi yangu yananiuma sana lakini kamwe hayata
nirudisha nyuma katika kutetea haki yangu! Namjua sugu na na ninajiua mm
ktk ubora wangu katika malezi ya mwanangu/ mm ni mama na si mama tu ni
mama bora kwa sasha na ananihitaji na sitamuacha na nyinyi wajinga
wachache endeleeni kuniponda na kuona na stahili kupata pigo hili na si
wote- kuna wengine wema kwa upande wangu na washukuru na nina waahidi
sitawarudisha nyuma nitasimama mpaka kieleweke- sasa hivi ni jasiri
kupita maelezo. In god we trust inshaalla.”
No comments:
Post a Comment