Kunani Kati ya Msanii Linah Na Kakake @zarithebosslady??? >>>>>>
Msanii wa muziki nchini Tanzania, anayefanya
vizuri katika muziki wa Bongo Fleva, Estelinah Sanga ‘Linah’, anadaiwa
kuwa kimahusiano ya kimapenzi na shemeji yake Mwanamuziki wa Bongo
Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ aitwaye William Bugeme ‘Boss Mtoto’ ambaye
ni kaka wa Zarina Hassan ‘Zari’ kiukoo.
Inadaiwa kuwa wawili hao
walionekana wakiwa sambaba ndani ya Ukumbi wa Triple 7 uliyopo Kawe
jijini Dar es Salaam, hivi karibuni na kugandana kama mtu na mpenzi wake
jambo lililozua maswali kibao kutoka kwa watu waliokuwemo ukumbini
humo. Sambamba na kuonekana katika ukumbi huo inadaiwa kuwa wawili hao
amekuwa wakionekana mara kadhaa wakiwa pamoja katika kumbi mbalimbali za
starehe jijini Dar es Salaam. Mara ya mwisho, Linah na Boss Mtoto
walionekana wakiwa pamoja kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo za Kili Music
zilizofanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam,
mapema mwezi huu
No comments:
Post a Comment