Ommy Dimpoz Ataja Umuhimu wa Meneja kwenye muziki wake >>>>>>
Ommy Dimpoz amesema mafanikio makubwa aliyonayo na kuweza kupenya kwenye
‘mainstream’, yametokana na kuelewa nini umuhimu wa kuwa na msaidizi na
msimamizi katika kazi zake na kumpa shavu meneja wake, Mubenga. Ommy
Dimpoz ameiambia E-News ya EATV kuwa alikuwa na mambo mengi ya kufanya
ambayo kama isingekuwa meneja asingeweza kuyafanya yote. “Nilipoamua
kufanya kazi kama solo
artist niliona umuhimu wa meneja maana mwanzo
kuna changamoto nilikuwa nazipata kama kufuatilia kazi zangu mwenyewe,”
amesema muimbaji huyo wa Wanjera. “Nilikuwa napata ugumu kipindi hicho
maana nilikuwa sina hata usafiri, nilikuwa napanda daladala. Unajua
foleni njiani unakuta hadi nilikuwa nachelewa mazoezi. Kipindi hicho
nipo katika band ndio maana nilivyoamua kuwa solo artist nilitambua hilo
ndio maana nikaamua kuongea tena na Mubenga ndio hadi nikatoa wimbo wa
“Nai Nai” pale tayari nilikuwa na nguvu ya meneja,” aliongeza.
No comments:
Post a Comment