CCM YABARIKI UBUNGE WA WEMA SEPETU >>>>>>
Siku chache baada ya mwanadada anayefanya
vizuri kwenye filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ kutangaza nia ya
kugombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), chama hicho kimempa
baraka mrembo huyo kwa uamuzi wake huo. Akistorisha na gazeti moja
nchini Tanzania, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema
kila mwanachama ana haki ya kugombea uongozi wowote ule ilimradi awe
mwanachama hai, hivyo kwa Wema kugombea ubunge wa viti maalum ni haki
yake na
amefanya uamuzi sahihi. “Kugombea uongozi ni haki ya kila
mwanachama, Wema ana haki, kwanza ni mwanachama hai na baba yake alikuwa
mwanachama mzuri sana wa CCM mpaka anafariki dunia, hivyo chama chetu
huwa hakikutani na watu barabarani tu, bali wanakuwa ni halali kabisa
mpaka wanatangaza kugombea,” alisema Nape. Hata hivyo, alisema wasanii
wote waliotangaza kugombea kupitia chama hicho hawajakurupuka bali ni
wanachama hai na wamekuwa wakishiriki kwenye shughuli mbalimbali za
kichama, tangu kwenye kampeni za mwaka 2010. Wasanii wengine
waliotangaza nia ya kugombea ubunge kupitia CCM licha ya Wema ni
Ndumbagwe Misayo ëTheaí (Viti Maalum, Kinondoni) na Wastara Juma (Viti
Maalum Morogoro Vijijini). GP.
No comments:
Post a Comment