Sijamponda Diamond, waandishi wananiwekea maneno mdomoni – Alikiba
Alikiba ameelezea
kusikitishwa kwake na taarifa iliyosambaa kuwa alitoa kauli dhidi ya
Diamond kuwa anajisikia kichefuchefu kila akimsikia msanii huyo.
Akizungumza na Bongo5 jana, Alikiba alisema hata watu wake wa karibu
wanajua hawezi kufanya jambo kama hilo. “Hiyo mimi nimeisoma juzi na
mwenyewe sijaifurahia. Vilevile na kibaya zaidi inaonesha eti kwamba
mimi nimesema nikimsikia Diamond najisikia kichefuchefu, mimi namchukia
Diamond,” amesema. “Yaani kwa uelewa wangu na akili yangu timamu hata
watu wanaonielewa mimi hata uwezo wa kusema hivyo sina na siwezi,
kibinadamu haipendezi. Halafu huyu mwandishi aliyeandika hivi
anamaanisha kabisa anapenda huu uchochezi ulipo na mabifubifu na mateam
team yanayoendelea ilimradi nionekane mimi na sura mbaya katika jamii.
Kwa sababu hicho kitu ni cha kutukosanisha. Huwezi kuniandika mimi
nimesema live halafu kulikuwa na waandishi wengine wakati nahojiwa mbona
hao waandishi wengine hawakuandika hivyo?” amehoji Kiba. “Ushahidi wa
sauti upo bana, sio kwamba unakwenda unaandika habari tofauti ilimradi
nionekane mimi ni mbaya mbele ya watu. Mimi hicho kitendo kimeniudhi na
sijakipenda, sijakifurahia na hii inakuwa inashusha hadhi ya kampuni kwa
sababu siku nyingine watu wanavyotaka habari tutaonyesha ushirikiano
mdogo kwa sababu ya vitu kama hivyo. Watu wanaalikwa vizuri kufanya kazi
ili kuwafikishia wananchi habari lakini habari zinazokwenda ni tofauti.
Hii haipendezi na sijafurahishwa nayo na nimesikia watu wanatukana sana
wanaongea comment tofauti tofauti.” alisema KIBA.
No comments:
Post a Comment