
fedha hizo huwa anatumiwa kwa njia ya simu na kudai kuwa Sugu, hatumi kwa tarehe maalum na kusema kuwa katika miezi sita iliyopita amemtumia fedha sio zaidi ya mara nne na sio kila mwezi kama alivyodai Mbunge huyo. Amedai kuwa Sugu alianza kulipa ada ya shule hivi karibuni, lakini mtoto huyo wa miaka miwili na miezi nane alianza kusoma akiwa na mwaka mmoja na miezi saba. Amesema kuwa kama kweli Mbunge huyo alikuwa anahitaji maridhiano angewashirikisha wazazi wake na ndugu zake kwa ujumla na sio kukimbilia mahakamani kama alivyofanya na kudai kuwa ni bora suala hilo likaamuliwe na mahakama kusudi haki itendeke.
No comments:
Post a Comment