Saturday, June 13, 2015

Godfather kuongoza video ya Yamoto Band, Diamond Platnumz Aigharamia >>>>>>>>

Meneja wa kundi hilo, Said Fella, amesema Yamoto Band watasafiri Jumatatu kuelekea nchini Afrika Kusini kushoot video hiyo. “Wiki ijayo tunatarajia kufanya video mpya ya Yamoto Band na Godfather atakuwa...director,” Fella ameiambia Bongo5. “Hatuendi south kama kuiga lakini madogo nao wanataka kwenda mbali zaidi.” “Tunajaribu kuwapenyeza zaidi Afrika. Kwahiyo Diamond ndio kaongea na Godfather na yeye ndo katoa hiyo ofa, hivyo hii ni ofa ya Nasib. Tunakwenda Jumatatu, tunafanya video Jumanne na Jumatano kuna shughuli tutaifanya tena,” alisema Fella.

No comments: