'Sitamtangaza mpenzi wangu kama maonyesho' Asema OMMY DIMPOZ>>>>>>>>>
MSANII wa muziki wa kizazi kipya
nchini Tanzania, Omary Nyembo aka ‘Ommy Dimpoz’, amesema hataki kuweka
wazi uhusiano wake wa kimapenzi na mpenzi wake kama wafanyavyo baadhi ya
wasanii ndani na nje ya Tanzania. Dimpoz alisema watakaomfahamu mpenzi
wake ni watu wake wa karibu na si kila shabiki
wake kwa kuwa mambo ya
mapenzi yanapendeza yakiwa siri. “Hakuna haja ya kufanya maonyesho ya
mapenzi kwa mashabiki, uhusiano wangu ni mimi na mpenzi wangu, hakuna
haja ya kila mtu kujua kwa sababu mapenzi si maonyesho,” alieleza msanii
huyo. Dimpoz alimaliza kwa kudai kwamba maisha yake binafsi yataendelea
kuwa binafsi na muziki wake ndiyo utakuwa kwa mashabiki zake wote kwa
kuwa unawahusu.
No comments:
Post a Comment