"Kama kuna Mwanaume Mwenye uthibitisho wa Kutembea na mimi si ajitokeze!” asema Wastara
Baada ya kuhusishwa kwa muda
mrefu na fununu za kutembea na wanaume kadhaa tangu kufariki kwa
aliyekuwa mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’, msanii wa filamu Bongo,
Wastara Juma hatimaye amefunguka na kujiapiza kwa kulamba kidole,
kuchovya mchanga na kukipitisha shingoni akidai tangu kuondoka kwa
Sajuki hajawahi ‘kuchangia shuka’ na mwanaume yeyote na kama yupo,
ajitokeze hadharani!
‘Akibadilishana sentensi’ na ‘kiruka’ njia wetu kwa
njia ya simu hivi karibuni, Wastara ambaye bado anafanya vyema kwenye
sanaa, alishutumu na kuonekana kuchukizwa vikali na tetesi juu yake
akihusishwa na wanaume kadhaa akiwemo msanii mwenzake, Bond Bin
Suleiman. “Nashangazwa sana na wanaoeneza uvumi wa mimi kutembea na
wanaume wengi baada ya kifo cha mume wangu, kwani mimi sina haki kama
mwanamke jamani? Kama kuna mwanaume mwenye uthibitisho wa kutembea na
mimi si ajitokeze!” alisema Wastara huku akiashiria jazba
No comments:
Post a Comment