Akizungumza kupitia kipindi cha “The playlist” cha “Times fm”, shilole amedai haoni sababu ya yeye

kujifunza Kingereza kwa kuwa sio lugha ambayo amekuta ikizungumzwa Tanzania.
“Mimi kingereza sio lugha yangu, mi nafanya tu nikipatia sawa nikikosea tu sawa, nikikosea Kiswahili waseme tu nakosea hadi Kiswahili, lakini kingereza sio lugha yangu kwa hiyo naongeaga basi tu sio lazima” alisema Shilole.
Kwenye line nyingine mmiliki huyo wa “malele”, amedai ndoto zake za kugombea Ubunge Igunga oktoba mwaka huu zipo kama kawaida, anachofanya kwa sasa anataka akomae kisiasa na “soon” atatangaza kuanza harakati hizo.
Credit:timesfmtz.com
No comments:
Post a Comment