
Amezungumza pia jinsi mwanzoni alivyokatishwa tamaa kwa wazo lake la Bongo Star Search, alivyotumia miaka mitatu kusaka mdhamini bila mafanikio, jinsi ambavyo alipata mshtuko mkubwa kuona mahudhurio ya kutisha kwenye audition ya kwanza kabisa jijini Dar es Salaam. Amezungumzia pia jinsi ambavyo alimuongeza Salama Jabir, @ecejay ambaye alishawishiwa naye baada ya kuidiss video ya muziki iliyoongozwa na kampuni ya Benchmark Productions.

Ameongelea pia msimu mpya wa shindano la @bongostarsearch.
Chill na Sky inasikika kupitia Kings FM ya Njombe (Jumatatu 10:45 hadi 11:45 jioni, na marudio Jumapili saa 5:00 asubuhi. Bomba FM Mbeya, Jumanne saa 9:00 Alasiri na Afya Radio 96.8, Mwanza, Jumatano saa 8:30 mchana kwenye The Beat Lab na kurudiwa Ijumaa saa 5:00 usiku kwenye Weekend Jump off na Jumapili saa 5:00 asubuhi kwenye Super Sunday.
Unaweza kusikiliza kipindi hapa chini
No comments:
Post a Comment