Jaffarai anaamini kuwa wasanii wa
zamani walilemazwa na muziki wa kipindi hicho kwakuwa ulikuwa unaenda
wenyewe tofauti na sasa hivi. Akizungumza kwenye kipindi cha Bongo Beats
cha Star TV, Jaffarai alisema kwa sasa muziki umebadilika na kuwa ni
zaidi kipaji. “Zamani mimi nilikuwa label pale Bongo Records, nyimbo
yangu ya Nipo Busy sijaipeleka redio,” alisema. “Zamani ulikuwa
ukishaisha studio umemeliza, utasikia tu nyimbo inapigwa Clouds,
inapigwa East Africa, yaani kila radio utasikia inapigwa.

Unajiuliza ile
imefikaje kule kumbe inapelekwa na maproducer wenyewe wanazituma,”
aliongeza. “Kwahiyo zamani wasanii hawakuwa wanapata tabu, ilikuwa ni
rahisi tu kuimba nyimbo kali inaenda, anakuja mtu wa video unafanya
hutoi hata hela, mtu anakuja anachukua DVD zako zinauzwa unapewa tu
pesa. Ile hali ililemaza sana watu, kwa sababu vitu vilikuwa vinaenda
vyenyewe. Sasa hivi mtu ukiwa na kipaji peke yake unafeli. Hata industry
imebadilika inahitaji mambo mengi. WasAnii wamekuwa wengi, muziki wa
sasa hivi unaHitaji update kila sehemu. Lakini zamani vitu vilikuwa
vinaenda vyenyewe automatic. Kwakuwa tulishazoa ile hali vitu
vimebadilika sasa hivi.”
No comments:
Post a Comment