Saturday, June 20, 2015

Nimefanya collabo na Msanii wa Afrika Magharibi aliyetwa kwenye MTVMAMA 2015' Asema Ben Pol.

Muimbaji wa Sophia, Ben Pol amesema amemshirikisha msanii wa Nigeria ambaye aliyetajwa kuwania tuzo za MTV MAMA 2015. Hata hivyo amedai kuwa kampuni inayomsimamia bado haijamruhusu kumweka wazi msanii huyo. “Labda nikupe hint, msanii ninayefanya naye ni mmoja wapo wa nominess wa MTV MAMA mwaka huu kutoka West Africa,” Ben aliiambia Djjonamusic Blog.
 
Amedai kuwa collabo hiyo inaweza kutoka mwezi ujao. “Tumeshamtumia muziki, ameshafanya kazi yake, kuna marekebisho kidogo, kuna Kiswahili kidogo tunataka tuweke ndio hicho peke yake kilichobaki,” aliongeza muimbaji huyo. “Ngoma beat amefanya Mswaki, yeye amerekodia kwao kule, vocals amefanyia kwao ametutumia lakini muziki umetengenezwa na Mswaki.” Ben Pol amesema kwa sasa anajipanga kufanya video ya wimbo huo na kwamba kwakuwa anayemshirikisha ni msanii mkubwa anatarajia kutoa video ya kubwa pia

No comments: