Wednesday, July 8, 2015

Fredrick Bundala:vyama vya upinzani itahitaji miaka mingi sana kuja kuweza kushika nafasi ya urais.

Mhalili mkuu wa mtandao wa Bongo5 ambaye pia alishawai kuwa mtangazaji wa kituo cha redio kinachomilikiwa na Sahara Communication Redio Free Africa RFA ameyaandika haya ikiwa ni tathmini yake anavyoiona kwenye vyama pinzani kupitia page yake ya facebook mapema hii leo, Soma alichokiandika hapo chini.

Mimi si mjuzi sana wa mambo ya siasa na huenda hoja yangu ikawa sio kweli lakini upepo ninaouona sasa ni kuwa upinzani itahitaji miaka mingi sana kuja kuweza kushika nafasi ya urais.
Upinzani wako slow sana yaani hasa katika muda huu ambapo wananchi wengi wana hamu ya kujua wagombea watakaopitishwa. Naona kabisa kuwa excitement kwenye mitaa, kwenye vyombo vya habari na hata kwenye mitandao ya kijamii ipo katika kutaka kujua CCM watamsimamisha nani kugombea urais.

 
Mbona mzuka huu haupo kwa kambi pinzani? Wao wanafanyaje stunts zao? Ni akina nani ambao wanatajwa sana kuwa wanaweza kuwa wagombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, CUF, TLP, NCCR – Mageuzi na vyama vingine? Mbona wao hawana stunts, hawatengenezi suspense, hana mbwembwe kabisa katika kipindi hiki? What’s their game plan? Wana surprise gani in stores? Au ndio mtaji ni mdogo kuweza kucheza stunts kama za chama tawala?
Nadhani wanahitaji kuchangamka zaidi. Wao pia watengeneze hamu hii ambayo CCM wamekuwa wakiitengeneza. Kama wataendelea na speed hii ya kobe, ikulu si sehemu watakayoingia mapema!!!

No comments: