Kala Jeremiah amesema kuwa wimbo wake ‘Nchi ya Ahadi’ aliomshirikisha Roma umempa shavu la kufanya kampeni ya kuhamasisha watanzania kushiriki
kikamilifu kwenye zoezi la kupiga kura katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Kala ameiambi Bongo5 kuwa atazunguka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania
ili kutoa elimu kwa watanzania kuhusu kutumia vitambulisho vyao vya
kupigia kura kuchagua viongozi
wanaowataka. “Kabla wimbo haujatoka
tulikuwa na mawazo ya kuingiza maneno ya kuhamasisha watu kupiga kura
lakini kwa bahati mbaya hatukuweza kufanya hivyo. Lakini baada ya kutoka
wimbo pamoja na video na kusambaa, Mungu sio athumani kuna tasisi
imenifuata ina idea ya kuhamasisha watu,” amesema. “Kwahiyo automatic
kwa kupitia ule wimbo, wakaona nilichokiimba kinafaa kuwa kwenye
harakati zao za kuhamasisha jamii kuhusu watu kujitokeza kwenye kupiga
kura baada ya kuona kuna baadhi ya watu wamejiandikisha ili wapate
vitambulisho kwa matumizi yao binafsi na si kupiga kura. Sasa sisi
tutaingia kati yao na kuzungumza nao juu ya umuhimu wa kura yao hata
kama kutakuwa na jua kali au mvua. Kwahiyo hiyo ndio deal iliyoingia
kupitia Nchi ya Ahadi.”
No comments:
Post a Comment