Salama Jabir na Solo Thang Watoa neno kwa team Kiba na Diamond >>>>>>>
Ushindani na upinzani unaokuzwa na
mashabiki kati ya makundi yanayojiita timu Diamond na timu Kiba, kwenye
mitandao ya kijamii umepelekea nyota wa sanaa nchini Tanzania,
kujitokeza hadharani na kuwaweka mashabiki sawa kwa kile walichokiamini
kuwa wamevuka mipaka kwenye ushabiki. Kutokana na sakata hilo la makundi
yasiyo na maana kwenye mitandao ya kijamii limepelekea mtangazaji wa TV
show ya Mkasi, Salama Jabir na msanii mkongwe bongo fleva, Solo Thang
kupaza sauti zao. Kupitia ukurasa wa
kijamii Salama Jabir, ameandika
“Wabongo tumekua wakosoaji mpaka wasanii wanajishtukia, hakuna “zuri
kabisa” kwenye macho yetu… tuwaache wasanii wawe “Wasanii” nadhani!”
Akaendelea “Jana tulikua tunaongea na wana job, Ali Kiba hakuwa mtu wa
vioo vikali, yeye alikuwa anatoa audio kali na video ya Mwananchi
kamaliza, zama zimebadilika mpaka anakwea pipa kwenda kutoa kideo
kikaaali tushukuru, kapendeza, rangi nzuri! mengine tuyaache..”.
Sambamba na hilo kutokana na maneno machafu ambayo yamekuwa yakitolewa
na timu hizo zimepelekea mkongwe wa Hip Hop nchini mwenye makazi yake
nje ya nchi Solo Thang, kuandika haya kwenye mtandao wa kijmaii “Ukiweka
habari au picha au muziki wa msanii muyu mashabiki wa yule
wanakutukana! kwanini? ? hii burudani tu isiwe uhasama, tujivunie sanaa
yetu”
No comments:
Post a Comment