Ukubwa wa muziki haupimwi kwa namna unavyochezwa redioni tena' – Godzilla >>>>>>>>>>
Rapper Godzilla amesema kuwa
kuna ngoma nyingi ambazo hazifanyi vizuri redioni lakini mtaani
zinapendwa na kusikilizwa na watu kwenye simu zao. Rapper huyo amedai
kuwa redio sio kipimo tena cha muziki kufanya vizuri kwa sasa. “Watu
wanazo nyimbo kwenye simu zao, wanadownload na kusikiliza,” Godzilla
ameiambia Djjonamusic Blog. “Ukiuweka kwenye internet watu wanadownload na kuwa
nazo, ndio muziki ulivyokuwa siku hizi. Ukitaka kujua hilo ni ukienda
kwenye show, watu wanaimba na wewe,” ameongeza. “Kwahiyo sasa hivi
ukubwa wa muziki haupimwi ni kwa jinsi gani umesikika kwenye redio au
kiasi gani cha rotation unapata, watu wanazo nyimbo kwenye simu zao.
Muziki umekuwa mpana kwamba watu wanaweza kupata muziki kwa njia nyingi,
kwenye internet, kutumiana kwenye whatsapp group kwahiyo watu wanazo
tu.”
No comments:
Post a Comment