"Ningependa wasanii tusaidie kutoa elimu ya upigaji kura kuliko kushabikia vyama" - Hemedy PHD
Hemedy PHD amedai hajajifunga na chama
chochote cha siasa kama ilivyo kwa wasanii wengi na kwamba jambo la
muhimu zaidi ambalo anaamini wangefanya ni kusaidia kueneza elimu ya
upigaji kura. Hemedy ameiambia Djjonamusic
kuwa wananchi wengi hawana elimu
hiyo na hapendi kuona limefumbiwa macho. “Wenye haki ya kupiga kura
tayari ni wengi, wengi wamekua na wengi ni wageni ambao wameingia kwenye
umri wa miaka 18 na kuendelea, tofauti na sisi tuliokuwepo before,”
amesema. “Nafikiri kuna haja ya watu kuelekezwa na kuelimishwa juu ya
upigaji kura, kwamba ukifanya hivi unapatia, hivi unakosea.” Hemedy
amesisitiza kuwa watu wengi pia hawajasoma na wana haki ya kupiga kura.
Anahofia kuwa kura nyingi zinaweza kuharibika kutokana na wananchi
kukosa elimu hiyo.
No comments:
Post a Comment