ROMA Asema hajapewa barua rasmi ya kufungiwa wimbo wake na BASATA
Rapper Roma Mkatoliki ameendelea kutawala
vichwa vya habari kufuatia sakata la kufungiwa kwa wimbo wake wa Viva
Roma Viva. Akizungumza kupitia Planet Bongo ya E A Radio, Roma amesema
kuwa yeye binafsi hajapokea barua rasmi ya kufungiwa wimbo wake kutoka
BASATA.
“Sina jibu la moja kwa moja na napata kigugumizi kwa sababu sina
taarifa rasmi kwa kweli, yani finaly mimi nakuwa kama shabiki tu tena,
vile shabiki alivyoona ndivyo mimi kama Roma nilivyoona, niliamka tu na
mimi nikaona kama kuna chombo kimoja cha habari kimepost katika akaunti
ya Instagram, kwamba kuna tamko limetoka BASATA kwamba limefungia nyimbo
ya Roma, kwa sababu ambazo walizianisha”. Aliongeza kuwa yeye hajui
utaratibu ambao BASATA inautumia kufikisha taarifa kama hizo kwa
wasanii. “Nisiwe muongo sijui taratibu kinakuwa kinatumia kufikisha
information zao, kwa sababu kitu ambacho naona ingekuwa rahisi kama
artist kabla hajaachia nyimbo yake mpya ama hajafanya kazi yake ya
sanaa, iwe inawasilishwa katika hiko chombo, nadhani hapo tungekuwa
tunaenda sawa.” Upande wa Afisa Habari wa BASATA, Bwana Aristide
Kwizela, alisema kuwa zipo njia mbili ambazo wanaweza kutumia kutoa
taarifa za namna hiyo. “Kuna kufungia kwa maana ya msanii mwenyewe
kuandikiwa, lakini kama kuna taarifa imetoka public kwamba nyimbo za
namna hiyo zimezuiliwa, kuna two way either barua kuandikwa kwa msanii
au pia kuna public anouncements kwamba wimbo fulani umefungiwa”, alisema
Kwizela.
No comments:
Post a Comment