Licha ya BASATA kutoa maelezo ya
jinsi ambavyo wanaweza kuufungia wimbo wa msanii kwa kutoa taarifa
kwenye vyombo vya habari pasipo kumwandikia msanii barua yoyote (Ingia
hapa ), Roma bado anaamini kuwa Baraza hilo la sanaa halijaufungia wimbo
wake. Akizungumza kupitia Planet Bongo ya EA Radio, Roma amesema kuwa
anaamini BASATA wanasapoti kazi zake hivyo taarifa za kuufungia wimbo
wake anazichukulia kama uvumi tu. “BASATA wanasapoti kazi za wasanii,
kwa hiyo huwezi kuniambia

kwamba wimbo wa Roma umefungiwa, BASATA
hawawezi kutoa maamuzi kama hayo ya kufungia ngoma ya Roma, me i’m sure
BASATA wanasapoti kazi ya sanaa na wanamsapoti Roma, na hizi taarifa
nazichukulia tu kama rumors,” alisema Roma. Rapper huyo ambaye amekuwa
kwenye headlines toka aachie wimbo mpya wa Viva Roma Viva (VRV)
ameendelea kusisitiza kuwa kinachomfanya aamini kuwa hajafungiwa ni
kwasababu hajapokea barua yoyote kutoka BASATA. “Kwanza hakuna Officia
letter ambayo nimepewa, pili nikiangalia mifano kama ambayo nimekupa na
vyenye ambavyo wao wamesema kwa mtazamo wao, hapana kwa chombo kama
BASATA hawawezi kuangalia kwa jicho hilo, mi nawaamini BASATA na najua
kabisa lazima wasapoti kazi zangu.” Alisema Roma. .
No comments:
Post a Comment