Mabeste
ameelezea sababu za kumtumia mke wake mke wake, Lisa kama video queen
kwenye Video yake mpya ‘Usiwe bubu’ inayotoka Ijuma hii, amesema mke
wake alikidhi vigezo vyote ambavyo director alivitaka. Mabeste
amefunguka hilo wakati anafanya mahojiano na kipindi cha Planet Bongo
cha ‘East Afrika Radio’

Amesema “Unajua director wakati anaisikiliza
nyimbo akawa anataka tu shoot, alikuwa anataka niwe na mwanamke ambaye
ni mke wangu, kwanza nikajaribu kutafuta nikaona sipati, nikapata wazo
nikaona vitu ambavyo anasema wife yuko navyo, alafu pia ili niwe
comfortable zaidi ya kile ninachokifanya, kwa sababu natakiwa ni act
kama mke wangu, nikaona kwa nini efort ambayo nataka niiweke kwa mtu
mwengine nisiweke wife, kwa hiyo ni kama kutoa kitu mfuko huu na
kuhamishia mfuko huu”
No comments:
Post a Comment