Wanamuziki wengi bado wanaishi lakini muziki umekufa – AFANDE SELE
Rapper mkongwe nchini, Seleman Msindi
maarufu kama Afande Sele, amesema wanamuziki wengi wanaweza kuwa hai
lakini muziki wao umekufa. Afande ameiambia Bongo5 kuwa muziki
umeingiliwa na wasanii wanaofanya biashara ya muziki bila kuwa na wito
na kazi hiyo. “Wanamuziki wengi wa zamani wa kizazi kipya
hata wale wa
zamani akina Mbaraka, Majani wametangulia mbele ya haki na wengine wapo
pamoja na wanamuziki wa kizazi kipya ambao hawajafariki dunia, lakini
kimuziki ni kama hawapo lakini nyimbo zao bado zinaishi. Ila wanamuziki
wa sasa hivi unakuta ndio wapo na vyombo vya habari vinawatangaza na
wapo kwenye peak za juu lakini bahati mbaya nyimbo zao haziishi hata
kidogo,” amesema. “Wanamuziki wengi bado wanaishi lakini muziki wao
umeshakufa. Lakini yote haya ni kwa sababu ya mtazamo wa kibiashara/ Leo
hii muziki umekuwa sio wito tena, kila mtu akiwa na mtaji wake anaingia
na anafanya poa. Kwahiyo sasa waandishi wa habari, wamiliki wa vyombo
vya habari pamoja na wadau wa muziki waangalie hili vinginevyo
hatusaidii kukua kwa muziki.”
No comments:
Post a Comment