PICHA:Ray C akirejesha kiuno chakekisicho na mfupa?
Huenda jitihada za Ray C kukirejesha
kiuno chake kisichokuwa na mfupa kimeanza kuzaa matunda!Kwa muda mrefu
muimbaji huyo amekuwa akijaribu kuupunguza unene wake
uliompoteza
muonekano wake wa zamani uliompa sifa jukwaani na sasa picha zake mpya
zinaonesha mafanikio. Muimbaji huyo ambaye jina lake halisi ni Rehema
Chalamila, ameshare picha zake mpya kuonesha hatua aliyofikia. “Haka ni
kanani???yaani sitaki kuamini haka katoto ni mimi uwiii !jamani nina
furaha sana moyoni kumuona ray c.wa miaka ile yaani acha tu!je nipungue
zaid au?sasa ndio muda wa kurudi rasmi kwenye muziki Babutale,
Mkubwafela dada yenu niko tayari sasa,” ameandika.
No comments:
Post a Comment