Tuesday, November 3, 2015

DMX amtupia lawama meneja wake wa zamani baada ya kushitakiwa kwa kosa la kutolipa pesa ya malezi

Rapper mkongwe, Earl Simmons aka  Dark Man X  amemtupia lawama meneja wake wa zamani kwa kutofanya wajibu wake ipasavyo hivyo kupelekea rapper huyo kuwekwa chini ya ulinzi kwasababu ya kutolipa pesa ya malezi ya watoto wake.
 
DMX ambaye hivi karibuni amerudi studio kwa ajili ya kutengeneza Album mpya, amedai kuwa suala hilo lilitakiwa liendeshwe kibiashara na meneja wake ndio alitakiwa alipe kwasababu anamfahamu mwanamke huyo ambaye ni mama wa watoto wanne kati ya 12 wa rapper huyo.

DMX aliwekwa chini ya ulinzi wiki iliyopita muda mchache baada ya kutoka jela kwakosa hilohilo la kutolipa pesa ya malezi kwa muda, Hata hivyo DMX ameachiwa huru na kesi hiyo imesogezwa hadi November 18.
Wakili wa DMX,  Jeffrey Chartier amesema “Lengo pekee hivi sasa ni kufanya kazi na kutimiza majukumu yake, na hii inampa fursa nzuri ya kufanya hivyo”

No comments: