Tuesday, November 3, 2015

Exclusive ya Mkurungenzi wa Endless Fame WEMA SEPETU ,

 usiku wa kuamkia leo aliweza kufanya kufuru ya aina yake kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa kwake iliyofanyikia ndani ya Ukumbi wa Wema Sepetu Hall, uliyopo ndani ya jengo jipya la Millenium Tower. 

 Katika Sherehe hiyo iliyokuwa imehudhuriwa na ndugu jamaa na marafiki zake ilifana kwa kiasi kikumbwa, ambapo Wema aliweza kupewa zawadi mbalimbali huku akionyesha zawadi yake ya gari jipya aina ya Range Rover la mwaka huu. Mbali na gari pia usiku huo meneja wake Martin Kadinda aliweza kuonyesha baadhi ya bidhaa zenye nembo ya Wema sepetu ambazo zitakuwa zikiuzwa kwenye duka lake lililopo Mwenge TRA.

No comments: