Boss wa MMG, RickRoss ameshinda kesi iliyokuwa inamkabili ya
kutishia kumpiga risasi na kumkufungia ndani aliyekuwa mfanyakazi wake,
Jonathan Zamudio.
RickRoss ambaye alikua anataumikia kifungo cha nje, ameshinda kesi
hiyo baada ya mahakama kufuta adhabu ya kutosafiri nje ya mji aliokuwa
anaishi, Jaji aliyekua anasimamia kesi hiyo amesema adhabu hiyo
imefutwa kwasababu aliyefungua kesi hiyo, Jonathan Zamudio haishi maeneo
ya karabu na Rapper huyo.
Mbali ya kesi hiyo kufutwa Rozay haruhusiwi kwenda karibu na maeneo
anayoishi kijana aliyemfungulia kesi na hatakiwi kuondoka mjini Georgia
bila kuoa taarifa.
No comments:
Post a Comment