Wednesday, November 4, 2015

Kuwa makini na haya mambo saba kwenye mtandao wa Facebook

Mitandao imekuwa kwa kiasi kikubwa sana,kila mtu anatumia account yake vile anavyojisikia, tukiacha Twitter,Instagram na Snapchat, Facebook ni mtandao unaotumika sana na ni kwasababu ni rahisi kutumia kuliko mitandao mingine, idadi ya watumiaji inaongezeka siku hadi siku vijana wadogo hata
 
wa shule za misingi nao wanajua kutumia mtandao huu, lakini je tunatumia mitandao vizuri inavyotakiwa au tunajua nini madhara ya kutumia mitandao ndiyo sivyo.
Kuna mambo ya kuzingatia unapo post vitu katika ukurasa wako wa facebook leo nitaongelea vitu saba muhimu ambavyo kila siku tunapost na hatujui kama inaweza ikawa tatizo kwetu  hasa kwa usalama wa kwetu na familia zetu .

  1. Anuani ya Nyumbani Kwenu/kwako
Wapo watu wanapiga picha nje ya mageti ya nyumbani kwao,wakati mwingine unapiga hata number ya nyumba yenu na hujui, watu kitu ambacho hawajui hizo taarifa unazoweka katika mtandao  zinaweza onekana na watu wengi hata wale ambao sio marafiki zako hii ni hatari kwa usalama wako na gamilia yako na wakati mwingine inaonekana kama ni kitu cha kawaida sana ila miaka inavyozidi kwenda mitandao inakuwa  na tekinologia pia na uhalifu pia utaongezeka.

  1. Taarifa za Ofisini kwako.
Kuandika unafanya wapi kazi pia ni tatizo, kama wapo watu wenye nia mbaya na wewe wanaweza kukufwatilia kwa kufwata tu taarifa zako za ofisi. Kama nilivyosema tekinologia inakuwa kwahiyo kitu cha muhimu kufanya ni kuhakikisha unaficha taarifa zako za karibu sana ambazo sio lazima watu wote wazione.
  1. Namba Yako ya Simu
Wapo watu wanaandika namba zao za simu kwenye taarifa za kuwahusu kwenye profile zako, unaweza kupigiwa simu na watu wengi wasio na maana, na hii wengi imewakuta wanapigiwa na watu hawawajui. Tumefikia wakati watu hatuaminiani na huarifu ni mwingi kwahiyo ni vizuri ukatoa namba yako ili isionekane na kila mtu.

  1. Mahusiano yako.
Kuna vitu sio muhimu kama   kubadili status kutoka single kwenda kwenye Relationship au engaged au married sio ishu sana, haijalishi utapata watu wangapi watakao comment kwenye profile yako, maisha yako yawe private kwako sio lazima kuonyesha dunia nzima unatoka na nani japokuwa hii ni fashion kwa watu wengi na kama hujampost mpenzi wako kwa wengine inakuiwa tatizo.

  1. Malipo yako.
Baadhi ya sifa zinaweza kuwaua watu, mtu kapata cheki ya pesa nyingi, basi ataipost facebook wapo watu wanapost pesa nyingi sana kwenye mitandao  hii inaweza ikawa ni hatari kwako na watu wanao kuzunguka  watu wanajifunza kutumia vizuri mitandao ikiwewo jinsi ya kutract mtu kutumia taarifa zake anazo tuma kwenye mitandao hii inaweza ikawa si sawa kwa usalama wako.

  1. Picha za Utupu
Kutuma picha za utumu ni tatizo, wapo watakao zitumia vibaya na hii itakupa sifa mbaya kwa jamii kwa wadada msijaribu kuwa kama kim kardashiana yeye anaweza kupata pesa nyingi kwa picha moja tu ya matiti yake. Mnatakiwa kujielewa na kama umeamua kufanya biashara kumbuka kuna sheria ya mitandao siku hizi.

  1. Hali yako na unavyojisikia.
Haina haja ya kusema kila unachojisikia kusema, japokuwa uhuru ni wako, kuna mambo mengine yanaweza kuwa siri yako, wapo wanaotumia mitandao ya kijamii kama diary ambayo anaandika kila kitu kuhusu maisha yake, usifanye watu wakusome maisha yako yote kwa kutumia tu ukurasa wako wa facebook.

No comments: