Thursday, November 19, 2015

Exclusive: Haya ndio mambo ambayo ALIKIBA anahisi kufanyiwa ili Asifanikiwe >>>>>

ALIKIBA aliishut down Instagram Jumatatu hii kwa post iliyozua maswali mengi. Wengi waliitafsiri post hiyo kama amelalamika kukosa tuzo za Afrima zilizotolewa Jumapili hii nchini Nigeria, licha ya kutajwa kwenye vipengele vinne. Akiongea na kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM kufafanua

kuhusu post hiyo ya Instagram iliyofutwa tayari, Kiba alisema aliamua kuandika hivyo kuwashukuru mashabiki wake kwa namna wanavyompigania na kuwahakikisha kuwa anajitahidi kwa nguvu zake zote kuwafurahisha lakini kuna mambo wasiyoyajua yanaendelea nyuma ya pazia.
“Sikuandika kwasababu ya tuzo, niliandika kutoa shukrani kwasababu walipiga kura lakini vile vile vitu ambavyo nafanyiwa mimi vingine sio vya kuvisambaza,” alisema.
Bongo5 imemtafuta mtu wa karibu kwenye uongozi wa Alikiba kutaka kujua kile ambacho wanahisi msanii wao anafanyiwa na wengi hawavijui.

Mtu huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe, alidai kuwa kuna watu ambao wamekuwa wakifanya kila wawezalo ili kuhakikisha kuwa Alikiba hafanikiwi kimataifa.
Ametolea mfano video za Mwana na Chekecha Cheketua pamoja na kuwa na viwango vinavyokubalika na kuongozwa na waongozaji mahiri barani Afrika, kituo cha MTV Base hakijawahi kuzicheza na wanapokuwa wakiuliza sababu wameshindwa kupewa maelezo yasioeleweka. “Tunawatumia MTV Base, video wanazipokea na wanatuma confirmation ya kuzipitisha lakini hatuelewi kwanini hawazichezi tena,” amesema. Amedai kuwa waliwapa Soundcity kipaumbele cha kucheza video ya Mwana kwa mara ya kwanza lakini baada ya hapo video hiyo haikuwahi kuchezwa tena. “Hata zile Top Ten East yao haikustahili kuingia kweli? Kuna video ngapi za Afrika Mashariki zinaingia kwenye top ten na zingine ni za kawaida tu iweje Mwana isichezwe?” amehoji. “Kinachoshangaza zaidi, kuna watu wanawaambiaga wasanii ukitaka kutoboa tobo kimataifa lazima upitie kwao.” Kwa mifano hiyo amedai kuwa Alikiba anahisi kuna watu wanaofanya kila njia hata kwa kumwaga fedha ili kuhakikisha kuwa jitihada anazozifanya hazifiki popote na kwamba kitu hicho kinamnyong’onyeza sana.

No comments: