
Tanzania kwenye album yao. Katika mahojiano waliyofanya na kipindi cha Mseto cha Radio Citizen na Willy M.Tuva mwezi August, 2015, Sauti Sol walisema kuwa kuna nyimbo walizowashirikisha Alikiba, Vanessa Mdee na Joh Makini, japo zote hazijaonekana kwenye album hiyo. Bongo5 imemtafuta Bien-Aimé Baraza ambaye ni mmoja wa waimbaji wa kundi hilo, kueleza kwanini hakuna wimbo hata mmoja kati ya hizo ulioingia kwenye album. Kitu cha kwanza ambacho Bien ameiambia Djjonamusic ni kuwa album ya ‘Live And Die In Afrika’ itakuwa na sehemu mbili, yaani Part 1 na Part 2.
Na sababu za wao kushindwa kuzijumuisha collabo hizo kwenye part 1 ni kuwa, kipindi wanakutana na Alikiba, Vanessa na Joh Makini, sehemu ya 1 ambayo ndio inatoka ilikuwa tayari imefanyiwa mixing na mastering na ikawa imeshapelekwa kuchapishwa.
Bien ameongeza kuwa pamoja na kuwa nyimbo hizo hazijaingia kwenye sehemu ya kwanza ya album lakini wataziachia kama singles, na collabo yao na Alikiba ndio itakayotangulia kutoka siku si nyingi. Bien alimaliza kwa kusema part 2 ya album hiyo ambayo itatoka baadae sana huenda mwakani, itakuwa ni ya collabo zote walizofanya zikiwemo za wasanii wa Tanzania, na zingine walizofanya na Tuface, Yemi Alade na wengine.
No comments:
Post a Comment