Thursday, November 19, 2015

Kazi Ya YAMOTO BAND Na DULLY SYKES Kuachiwa Rasmi Hapo Kesho >>>>>

Nguli wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania na Afrika Mashariki Prince Dully Sykes Pamoja Na Vijana machachari kutoka Band ya YAMOTO Watakuwa Wanaachia Collabo Yao Hapo Kesho Siku Ya Ijumaa Kwenye Kipindi Cha Friday Night Live. Akizungumza hivi Majuzi katika segment

ya 255 kupitia XXL ya Cloudsfm na Perfect Crispin @perfectcrispin, Dully alisema kuwa ngoma hiyo ipo tayari na Yamoto wameshiriki katika Kuiandika ngoma hiyo aliyoipa Jina la TUACHIE
"Yah nyimbo iko tayari.. Video pia ipo tayari na imefanywa na Director HASCANA. Na nimeifanya ki Afrika zaidi, naamini itafika mbali sana, pia Hanscana amejitahidi Sana. Nyimbo imeandikwa na wadogo zangu YAMOTO, niliwaomba waiandike sababu kiukweli vijana wako vizuri." alisema Dully.

No comments: